WaWAZAZI SIMAMIENI MAADILI KUPUNGUZA UDHALILISHAJI KWA WATOTO MIAKA 15 NA KUENDELEA.
- Get link
- X
- Other Apps
wazazi na walezi Nchini wameaswa kusimamia maadili na kuwalinda watoto dhidi y vitendo vya udhalilishaji vinavyojitokeza kutokana na sababu mbali mbali katika jamii zao .
Ameyasema hayo Kamishna wa polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad alipokuwa akizungumza na wananchi huko katika uwanja wa Mpira Kendwa wilaya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba katika mkutano maalum wa kushajihisha ulinzi sirikishi katika shehia za kendwa na kiwani.
KAMISHNA POLISI ZANZIBAR HAMAD KHAMIS HAMAD
Amesema moja ya sababu zinzazopelekea watoto kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ni pamoja na kukosa maadili na malezi bora hususan kwa watoto ambao tayari wamefikia umri wa miaka 15 na kuendelea jambo ambalo hupelekea kujiingiza katika tabia hatarishi.
"Wazazi mnajukumu kubwa la kusimamia maadili ya watoto wenu wakike na wakiume haswa wale ambao umri wao ni hatarishi wanajiingiza katika tabia mbaya kutokana na kutokuwafuatilia nyenendo zao ".
Aliwataka wazazi hao pia kuendelea kufuatilia nyendo za watoto wao na kuwachukulia hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuwakanya endapo watabaini kujihusisha na tabia mbaya.
" Tusione wamekuwa watoto na kuwaachia mamlaka ya kujiongoza wenyewe watafanya wanavyotaka bila kujali kuwa wanapotea kila mzazi wajibu wake ni kumchunga mtoto wake dhidi ya vitendo viovu wanavyofanya wao kwa wao lakini pia wanavyifanyiwa na watu ambao hawana aibu kufanya udhalilishaji kwa watoto".
Aidha Amewataka wananchi haobkusimmka suala la mporomoko wa maadili pamoja kuwashirikisha viongozi wa dini katika kulifanikisha suala hilo.
"Viongozi wa dini maimu katik misikiti yetu licha ya kulikumbusha suala hili lkini pia tunayo nafasi kubwa kuanzisha kamati maalum za kusimamia maadili katika kusaidia vizazi vyetu visivunje maadili".
Katika hatua nyengine Kamishna Hamad amewataka wananchi wa kendwa na kiwani kutoa mashirikino kwa ulinzi shirikishi katika kudhibiti vitendo vya kihalifu ikiwemo wizi wa mazao na mifugo katika shehia zao.
"Endapo wananchi tutatoa mashirikiano kwa wenzetu hawa walioamua kusaidia kuimarisha ulinzi katika shehia na vijiji vyetu wizi wa mazao pamoja na mifugo hata wizi ule wa kudokoa majumbani hautokuwepo".
Lakini tukiona ni jambo la kawaida kesho kakamatwa mtoto wa fulani Kachukuliwa hatua mzazi wake kaja juu hatutofika popote na uhalifu utaendelea". Aliendelea Kamishna.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi
Mkutano huo wa kuhamasisha mashirikiano kwa wanajamii katika ulinzi shirikishi Yalikutanisha wananchi wa vijiji mbali mbali vilivyomo katika shehia za kendwa na kiwani.
kwa upande wa wananchi wamemshukuru Kamishna ambapo wamesema kuwa kunzishwa kwa vikundi hivyo kutasaidia kupunguza vitendo vya kihalifu katika vijiji vyao.
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment