WATUMISHI WA UMMA PEMBA WAPEWA USHAURI KUBORESHA UTENDAJI KAZI.

Na Amina Ahmed

Waziri wa Nchi ofisi ya raisi  tawala  za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz   Massoud Ali Muhammed  Ameagiza  Maafisa Watumishi  wa  taasisi mbali mbali zilizo chini ya wizara hiyo  kisiwan pemba kufanya uhakiki na kujua  ongezeko la watumishi ambao  majukumu  yao  yanaendana  sawa katika  taasisi zao na kuwahamishia taasisi ambazo zina upungufu  wa watumishi hao si zaidi wiki moja kutoka  sasa. 

 Ametoa agizo hilo  Huko katika ukumbi za wizara hiyo Wawi  Chake Chake Pemba   alipokuwa akizungumza na  wakuu wa taasisi  mpoja na maofisa watumishi   katika kikao kazi  cha wizara hiyo mapema Leo Asubuhi. 
Massoud Ali Muhammed 
Waziri Tamisemi Zanzibar. 
Amesema  kumekuwa na mrundikano wa watumishi  ambao wana majukumu sawa katika  baadhi ya taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo  huku baadhi  ya taasisi nyengine  zikikosa Watumishi   kutokana na kukosa watendaji wenye sifa  kutokana na waliowengi kukaa sehemu moja na kurudisha nyuma  shughuli zautendaji kazi. 

 "Natoa wiki moja kwa  maafisa utumishi  mtathmini wengi   na kulifanyia kazi suala hili sio kazi ya  mtu mmoja wanafanya watu wanne watano  ndio wanafanya nataka lishughulikiwe mara moja   waondolewe wengine wapelekwe ambako hakuna   wakafanye kazi wasikae tu  huko wakaishia kutowajibika Alisema Waziri Massoud  kila sehemu nataka nikute wafanya kazi  wanawaibika sio nifike baadhi ya maeneo watumishi hakuna. "


Aidha  waziri huyo ameagiza  wakuu wa taasisi na watendaji hao Kuandaa mafunzo maalum  kwa wafanya kazi wa wizara hiyo  kila baada ya muda ili kuwasaidia kuzidisha ufanisi na kutambua majukumu miiko na maadili ya  ya kazi zao. 

" Ni jambo La kusikitisha  Mtumishi wa wizara kutojuwa wajibu wake kutojua vipi anatakiwa avae,  kutokujua haki zake kama mtumishi   ni zipi naagiza   kuliangalia suala hili kwa kuandaa mafunzo kila baada ya muda kwa watumishi  tunataka  watumishi bora sio bora watumishi". 

 Aidha amewataka  watendaji na maofisa hao kutosita kuchukua hatua za kinidhamu  kwa watumishi ambao wanakwenda kinyume  na sheria za kazi kwa kukiuka  sheria     pamoja na kutoa taarifa endapo watakuwa nahofu ya kuwawajibisha. 

" Mkiona mtendaji awe baraza la mji halmashauri wete mkoni chake na kwengineko  anakiuka maadili mnamuwajibisha hawajibiki msisite  kushirikisha viongozi wa juu   kma ni naibu katibu hata mimi ambae nina dhaman nitamuwajibisha   kwa makosa yakekama ni uhamisho kumsimamisha au hata kumfukuza  lakini  muwawajibishe  endapo watakuwa  wanatenda mambo ya ovyo alisema. ". 


Aidha  Massoud  amewaasa maafisa utumishi kutoa mashirikiano  mazuri kwa wafanya kazi na kuacha kutumia  lugha chafu  zisizo stahiki  . 

" Nataka muwe na ukaribu katika   kesi ndogo ndogo muwe mnazitatua  ni jambo la aibu mfanya kazi kukosa mashirikiano kunitafuta mimi  kunilalamikia  hata kesi ndogo tu  mfani ya stahiki yake ya likizo na mambo mengine wakati watendaji  dhamana  wapo huku, nataka iwe  mfano   bora katika mashirikiano sio  maafisa mjione nyniy ndio bora kuliko wengine  waliooo chini yenu kila mmoja ajuwe ni mtumishi wa umma ".

Alindelea kusema kuwa endapo ofisi haitokuwa na mashirikiano  uwajibikaji na utendaji kazi hautoimarika kwani kila mtu hatokuwa na nifhamu ya utendaji kazi. 

  Akizungumza   katika kikao hicho Ofisa mdhamini wizara ya nchi ofisi ya raisi tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz Thabit Othman Ali  amemshukuru Waziri huyo   kwa  kuwakumbusha zaidi wajibu na  utendaji  kazi wao  ambpoa amesema kuwa    wizara hiyo kisiwani pemba itazidisha  mashirikiano  katika kusimamia utendaji kazi kwa watumishi wake   sambamba  na kuyafanyia  kazi maagizo  aliyoyatoa . 
Kishoto Ofisa Mdhamini wizara ya nchi ofisi ya raisi tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz 
Thabit Othman Ali. 

Mwisho


Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.