WANAOKUSANYA KODI WAMEOMBWA KUZIDISHA KASI

Na Maryam Hamad 

Naibu Waziri Ofisi ya rais Fedha  na Mipango Zanzibar  Ali Sleiman Ameir  amewataka   watendaji  na wasimamizi   wa  ukusanyaji   kodi   Pemba  kuongeza kasi katika sula hilo sambamba na kulifanya  kuwa endelevu katika kufikia malengo  ya upatikanaji wa mapato katika vianzio mbali mbali  .
 
ALI SLEIMAN  AMEIR
 Naibu  Waziri Ofisi Ya Rais Fedha Na Mipango Zanzibar 

 Ameyasema  hayo  Alipokuwa akizungumza na  na watendaji wa wizara na tasisi  za serikali ,makatibu  tawala  wilaya na mkoa   ,watendaji wa mabaraza ya miji na halmashauri , Tra,ZRB ,wakala wa serikali mtandao  pamoja na wakuu  wa taasisi zinazojitegemea  kisiwani humo  katika kikao kazi  kinachohusu  mikakati  ya kufikia  makusanyo  kwa mwaka 2022,23  huko katika ukumbi wa wizara hiyo Gombani chake chake.

Amesema  endapo watendaji hao  watashirikiana  pamoja katika suala hilo  mpango wa makusanyo na mapato utakuwa endelevu na wenye kuleta maendeleo kwa wananchi na serikali .

Awali akizungumza  na watendaji   pamoja na  wasimamizi hao   naibu katibu mkuu ofisi ya rais fedha na mipango Zanzibar Aboud Hassan Mwinyi  amesema   kila mmoja  ana wajibu wa kushajihisha suala  la ulipaji kodi pamoja kudai risiti kwa wafanya biashara.

 Kwa upande wake ofisa  mdhamini  ofisi ya rais fedha na mipango  Abdul wahab said abuubakar  amesema wizara hiyo itaendelea kushirikiana na watendaji  na taasisi zinazohusika na  ukusanyaji wa mapato   kisiwani pemba ili kufikia malengo yaliowekwa   na serikali  katika kupata makusanyo yaliokusudiwa kufikiwa kwa mwaka.

Kikao kazi hicho  kiliwashirikisha watendaji waofisi ya  rais  fedha  na mipango pemba, wasimamiz pamoja na taasisi zinazohusika na ukusanyaji wa kodi , makusanyo na mapato    katika maeneo mbali mbali kusini na kaskazini pemba.
mwisho

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.