WANANCHI TOENI MASHIRIKIANO KUDHIBITI VITENDO VYA UHALIFU.
Na Amina Ahmed
Kamishna Wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema Jeshi la Polisi litaendelea Kutoa Mashirikiano Katika kutatua changamoto za kihalifu zinazojitokeza katika shehia Mbali Mbali kwa kushirikiana na ulinzi shirikishi katika shehia hizo ili kudhibiti na kumaliza vitendo hivyo.
KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR
HAMAD KHAMIS HAMAD
Ameyasema Hayo Alipokuwa Akizungumza na Masheha wa shehia za Mkoa wa kusini Pemba, Viongozi wa dini Askari wakaguzi pamoja na maafisa Ustawi wa jamii katika ukumbi wa Polisi Madungu Chake Chake katika mkutano maalum wa kujitambulisha pamoja na kusikiliza changamoto kwa shehia ikiwa ni siku chache baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo Visiwani Zanzibar
Amesema kuimarisha ulinzi na usalama ndio nyenzo pekee itakayosaidia wananchi kuweza kufanya shughuli zao za kuleta maendeleo wakiwa katika hali ya utulivu.
"Mwalimu ataweza kusomesha Daktari ataweza kutibu mfanya biashara atakuwa huru kufanya biashara na kila kitu katika nchi kitakwenda vyema endapo tutakuwa na mashirikiano katika kudhibiti vitendo hivi jeshi la polisi linahitaji mashirikiano yenu kulifanikisha hili Tutamia mbinu zetu kama watendaji wa jeshi kulifanikisha hilo".
Alisema kuwa masheha viongozi wa dini na maafisa ustawi pamoja na wananchi wanafahamu
Zaidi Changamoto zipi zinapelekea uhalifu katika maeneo yao hivyo ni vuema kushirikisha jeshi la polisi katika kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.
" Msiogope kuwashirikisha askari polisi katika kudhibiti uhalifu katika Shehia Zenu toeni taarifa kwa maafisa wakaguzi askari wa wilaya mkoa hata ikiwezekana kwangu mimi matukio au viashiria vyivyote vya uhalifu tutaafanyia kazi".
Aidha Kamishna Hamad Amewataka masheha kuwatambua wageni wanaoingia katika shehia zao n kutoa taarifa endapo watakuwa na hofu juu ya mgeni yeyote ili kudhibiti vitendo vya uhalifu kutokana na muingiliano huo wa watu wenye tabia mbali mbali.
"Asilimia Kubwa Wananchi katika vijiji wanajuana tabia zao masheha utaratubu wa wa kuwatambua wageni wanaoingia na kutoka katika shehia musiupuuze ni moja kati ya sababu zinazopelekea kujitokeza matendo hayo maovu".
Wakizungumza Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kwa upande wa masheha, Sheha wa shehia Madungu Mafunda Hamad Rubea Pamoja Ali khamis Massoud Sheha wa shehi ya mvumoni wamemuomba Kamishna huyo Kushirikisha Vikosi vyengine vya Polisi vilivyopo Zanzibar Katika kuendeleza maoambano ya kudhibiti uhalifu .
"Kuna kipindi tuliona vikosi vyite vinafanya kazi kwa pamoja sasa ule wingi wao wahakifu unawatia hofu wanapunguza matabia yao lakini lei shehi nzima askri mmoja ikifika jioni anarudi kwakwe hawatogopa tunomba mrudishe yale mambo alisema Ali khamis".
Kwa upande wao viongozi wa dini Akiwemo Robert Migue kiongozi wa dini katika kamati ya dini wilya ya chake chake Pamoja na Hamad Shaame Hamad wameliomba jeshi hilo kuwapatia mafunzo ya vitendo askari jamii walioamua kujitolea kusaidia ulinzi katika shehia na vijiji vyao.
" Tunapata madhila sana sisi ambao tumejitolea kudhibiti wahalifu lakini inafikia hatua moka mtu anapomkamata muhalifu anatafunwa anabaki na kovu atakwenda nazo kaburini hii ni kutokana na kukosa uelewa na mbinu za kupambana nao tunaomba uliangaie hilo moite katika shehia vikundi vya ulinzi shirikishi muvipatie mafunzo"Alisema sheh shaame.
Katika mkutano huo mambo Mbali Mbali Yalishauriwa katika kuimarisha ulinzi na kupunguza vitendo vya uhalifu Kusini Pemba ambapo awali Kamishna huyo alizungumza na masheha mkoa wa kaskazini Pemba huku akitarajiwa kuzungumza na viongozi wa siasa Mkoa huo Mapema Kesho.
Mwisho
Comments
Post a Comment