WAALIMU PEMBA ONGEZENI BIDII KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM.
NA FATMA SLEIMAN ABRAHMAN .
Walimu kisiwani Pemba wametakiwa kuwasimamia ipasavyo maendeleo ya wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na kuondoa kasoro zilizopo ili kuongeza kiwango cha ufaulu wao wakati wa mitihani ya taifa visiwani zanzbar .
Hayo yameelezwa na afisa mdhamin wa wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba Mohd Nassor Salim wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa walimu yaliofanyika katika ukumbi wa TC michakaini amesema Zanzibar katika utekelezaji wa elimu mjumuisho unakwenda vizuri hivyo ni jukumu la walimu kuongeza bidii ili kuhakikisha kila mmoja anapata elimu bora na ufaulu kuongezeka .
AFISA MDHAMINI WIZARA YA ELIMU PEMBA.
MUHAMED NASSOR SALUM.
Akitoa elimu kwa walimu hao mratib wa baraza la mitihani mwalim Mohd Abrahman Shehe amesema elimu ambayo wameitoa kwa walimu itaweza kuwasaidia kuwatambua kwa urahisi wanafunzi ambao wanamahitaji maalum ili kuweza kupatiwa elimu kulingana na uwezo wao
Nao walimu waliopatiwa mafunzo hayo wameishukuru serekali kwa kupitia wizara ya elimu kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani wanatarajia kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
Mafunzo hayo ya siku mbili kwa walimu wawakilishi wa wanafuzi wenye mahitaji maalum kisiwani Pemba ambayo yametolewa na baraza la mitihani kwa lengo la kumuendeleza kitaaluma
Comments
Post a Comment