UHABA WA VITUO VYA POLISI WILAYA YA CHAKE CHAKE BADO MLIMA MREFU KUDHIBITI UHALIFU VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAMU.
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA CHAKE Chake ni moja kati ya wilaya mbilizi zinazopatikana katika Mkoa wa Kusini Pemba Zanzibar Tanzania. Ambayo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ina idadi ya wakaazi 97,249 na anuani za makazi zikiwa ni 74200 Idadi Mpya ya wakaazi wa Chake Chake kwa takwimu za Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 iliyotolewa hivi karibuni bado hazijapokelewa katika ngazi za wilaya ni kutokana na takwimu hizo kuikiishia katika ngazi za Mikoa pekee jambo ambalo limewia ugumu kupatikana idadi mpya ya wakazi wake wa sasa. Chake Chake ina jumla ya shehia 32 ambazo wakaazi wake hulazimika kutumia kituo kimoja pekee cha polisi katika kuripoti matukio mbali mbali. Matukio hayo ni pamoja uhalifu, udhalilishaji wa kijinsia wazee wanawake na watoto, wizi wa mazao , mifu...
Comments
Post a Comment