Katika miaka ya mwanzo ya maisha ya mtoto ndipo msingi mkubwa wa ukuaji wake hujengwa. Mtoto mdogo anahitaji mazingira yatakayomsaidia kukuza akili, afya, hisia na uwezo wa kuwasiliana na watu wanaomzunguka. Vituo vya TUTU vimekuwa sehemu muhimu katika kuhakikisha watoto wa umri wa awali wanapata malezi na elimu inayowaandaa kwa maisha yao ya baadaye. Najua bado unajiuliza Tutu ni nini lakini kamwe katika masikio lako sio neon geni TUTU ni kifupi kinachotumika kumaanisha Taaluma ya Uangalizi na Ujifunzaji wa Watoto Wadogo. Vituo vya TUTU ni sehemu maalumu zinazotoa malezi, uangalizi na elimu ya awali kwa watoto wadogo kabla ya kuanza elimu rasmi ya msingi. Vituo hivi vinalenga kumsaidia mtoto kukua vizuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo ukuaji wa akili, lugha, afya, hisia, tabia na mahusiano na watoto wengine. Katika vituo vya TUTU watoto hujifunza kupitia michezo, nyimbo, hadithi, mazoezi ya ubunifu na shughuli zinazolingana na umri wao. Lengo kubwa la TUTU ni kuhakikisha ...
MTANDAO wa Asasi za kiraia wa Pemba (PACSO) umeandaa mkutano maalumu kwa wananchi wa Kisiwa kidogo cha Kojani wenye lengo la kuiwezesha jamii kupata uwelewa mpana juu ya masuala ya kisheria na haki za binaadamu. Mkutano huo uliowashirikisha wananchi wa Kisiwa cha Kojani umeandaliwa na jumuiya PACSO kwa ufadhili wa shirika la UNDP na kufanyika huko ukumbi wa skuli ya msingi Kisiwani humo. Akizungumza na wananchi Mkurugenzi Mkuu wa PACSO Pemba Mohamed Najim Omar katika mkutano huo alisema, mpango huo una lengo la kuiwezesha jamii kupata ufahamu wa kisheria na haki za binaadamu. "Jamii zetu bado zina changamoto nyingi na baada ya kuliona hili tumeamua kuandaa mpango wa kupita kwenye jamii kutoa taaluma ya kuwawezesha watu ufahamu juu mambo haya, elimu zinatolewa nyingi lakini na sisi pia tumeona kuja haja ya kuwafikia", alisema. Aidha alisema, kutokana na kujitokeza masuala mbali mbali ya unyanyasaji wa kijinsia, watoto kudhalilishwa, wanawake, watu wenye ulemavu na hata wazee ...
SALMA KHMIS - UNGUJA KATIKA Uongozi wa taifa hili viongozi ambao wako karibu na wananchi na wanapaswa kuhakikisha maendeleo yanafikiwa na yanafanyika ni Masheha. Masheha wa Wilaya ya Magharib B wamejipanga kuhakikisha maendeleo na mabadiliko yanapatikana ndani ya shehia zao. Wilaya ya Magharibi B ni miongoni mwa Wilaya tatu zilizomo katika mkoa wa mjini magharib Unguja ambapo Mkoa huo una jumla ya masheha 121 kati ya hao 19 ni wanawake na 101 ni wanaume. Wilaya ya Magharibi B ni Wilaya iliyotoa shehia 34 kati ya hizo shehia 6 zinaongozwa na masheha wanawake na shehia 28 zinaongwa na masheha wanaume. Shehia ya kijitoupele na michungwani ni Shehia maarufu zilizomo katika Wilaya ya Magharib B ambazo zinaongozwa na Masheha wanawake. Shehia hizo kwa kiasi kikubwa zimepiga hatua za kimaendeleo ikiwemo kueka mazingira safi na kupambana na vitendo vya uchimbaji wa ...
Comments
Post a Comment