Masheha Kusini Pemba Wapewa Neno
Na Amina Ahmed
Waziri wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amewata msheha a Wa mkoa wa Kusini Pemba kuendelea kuhimiza wananchi juu ya kusajii kupata na kutumia Kadi za matibabu ya afya ili kuendana na mpango wa serikali katika kuboresha huduma za afya.
Waziri Wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui.
Ametoa wato Huo Wakati kizungumza na masheha wakurugenzi wa baraza la mji Chake na Mkoani, makatibu tawala wa wilaya n mkoa wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama katika mkutano wa kushajihisha na kuhamasisha matumizi ya kadi za afya kwa wanachi.
Amesema Bado Serikali hairidhishwi n mfumo wa matibabu uliopo kwa sasa hivyo mfumo huo wa kutumia kitambulisho cha matibabu utasaidia wananchi kuweza kupata mtibabu sahihi na kwa wakati.
Aidha Waziri Mazrui amewataka watoa huduma kudhibiti taarifa za kadi hizo kwa kuzijaza katika mfumo wakielectroniki pamoja na kuacha tabia kupuuza kuzisajili zinapofika katika vituo vya fya.
Akizungumza umuhimu wa kadi hizo masheha wa Shirika la PharmAccess Faundation Faidha Ali
amesema mfumo huo utasaidia kupata huduma bora zaidi za afya hususan ni wale watu wenye vipato vya hali ya c
Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud Amelipongeza shirika la Pharm Access Faundation kwa kuisaidia serikali kusaidia huduma za matibabu ambapo ameahidi kushirikiana na msheha hao katika kulifanikisha suala la upatikanaji wa kadi za matibabu kwa wananchi wa mkoa huo na kukamilika kw wakati sahihi uliowekwa.
Mwisho
Comments
Post a Comment