Posts

Showing posts from December, 2023

23 KUZINDULIWA KUSINI PEMBA

Image
Na Thureya Ghalib ,Pemba. Jumla ya Miradi 23 inatarajiwa kufunguliwa kuzinduiwa pamoja  na kuekewa mawe ya msingi katika Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni shamra shamra za kuekelea kilele cha Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar . Hayo yamelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari huko ofisini kwake Wilaya ya Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Mattar amesema miradi 10 itafunguliwa katika Mkoa huo ,miradi 4 itazinduliwa na miradi  9 itaekewa mawe ya msingi ,ambayo inahusu masuala ya maendeleo ya Wananchi . Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Wananchi kushirikiana katika shughuli zote ,kwani sherehe hizo hasihusiani na masuala ya kisiasa au itikadi zozote. Pamoja na hayo ametoa Wito kwa Wananchi kushiriki katika shughuli za Usafi hapo Kesho ,kwani Usafi ni Afya na unaondosha Maradhi mbalimbali.                               ...

Mwanamke awapika wenzake kuwa viongozi

Image
 Na Thuwaiba Habibu Elimu  ni mchakato wa kupata ujuzi, kukuza uwezo wa kifikiri na uamuzi na kujitayarisha  kiakili kwa maisha bora. Elimu pia hutoa muongozo wa kumuwezesha mtu kufanya jambo kwa vizuri zaidi na humpa mtu uwezo wa kuwaongoza wenzake. Vile vile humpa mtu uelewa wa kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya biashara au jambo jengine litalomuwezesha kujiongezea kipato  na hata kujiepusha na maradhi au hatari inayoweza kuathiri maisha yake. Nchi nayo hufaidika kwa kujipatia maendeleo pale ambapo watu wake huwa walioelimika Katika kijiji cha Bumbwini Makoba, wilaya ya Kaskazini B, Unguja, lilikuwepo kundi kubwa la akaina mama waliokuwa hawana elimu hata ya kusoma na kuandika. Hali hii iliwaweka nyuma na kutoweza kuwa viongozi, lakini pia hata sauti zao kutosikika kwa mambo yanayowahusu katika maisha yao ya kila siku. Kutokana na  hali ya kuelewa kwamba palikuwa panahitajika  elimu ili kuibadili taswira hio ndio kilichompelekea Bi Shida ...

WANANCHI WAHOFIA USALAMA WA AFYA ZAO UKOSEFU WA ENEO MAALUM LA KUCHOMEA TAKA ZA HOSPITALI PEMBA.

Image
NA, KHADIJA ALI YUSSUF-PEMBA.  SERA ya Wizara ya Afya ya 1990, imesema itahakikisha inaimarisha miundo mbinu mbali mbali Hospitalini ikiwemo Dawa, Usafiri, Mashimo ya kuekea Taka, pamoja na huduma za Mama na mtoto, ili kuondosha usumbufu kwa wananchi wake. Lakini licha ya hilo bado kuna baadhi ya vituo vya Afya, vimekuwa vikilalamikiwa kutokana na kukosa miundombinu rafiki hususan, Mashimo ya kuchomea taka na kupelekea athari kwa wafanya kazi wa vituo hivyo pamoja na wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya vituo hivyo vya Afya. Kukosekana kwa matanuri maalum ya kuchomea taka kwa baadhi ya hospitali Kisiwani Pemba kunasababisha kuathiri afya za wananchi waliopo karibu na hospitali hizo. Hayo yamejiri baada ya mwandishi wa habari hizi, kutembelea baadhi ya vituo sita  kisiwa Pemba, ikiwa ni pamoja na kituo cha Afya Bagamoyo, Wesha, Pujini,Vikunguni, Mgelema na Mbuzini na kubaini changamoto  ya vituo hivyo kukosa sehemu maalumu ya kuchomea taka na kupelekea kero k...

MABADILIKO WATENDAJI ZRA PEMBA WALETA MATUMAINI KWA WAFANYA BIASHARA

Image
NA, AMINA AHMED MOH’D - PEMBA.  BAADHI ya Wafanya Biashara  wilaya ya  Mkoani  mkoa wa Kusini Pemba wamepongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA  juu ya maswala ya utolewaji wa  elimuya kodi  na hatua za ukusanyaji wa mapato   ukilinganisha  miaka iliyopita.    Kauli  hizo zimetolewa na wafanya biashara  kutoka mitaa na maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo   walipokuwa wakizungumza  mbele ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA Pemba Jamal Hassan Jamal aliefika  ndani ya wilaya hiyo   kuzungumza na kusikiliza changamoto za wafanyabiashara maeneo tofauti ikiwa ni mwezi maalum wa kurejesha shukurani kwa walipa kodi ulioandaliwa na  mamlaka hiyo.  Wamesema suala la utolewaji wa taaluma juu ya njia  sahihi za ulipaji kodi zimeimarika na jambo ambalo awali lilikuwa  ni changamoto kubwa  kwa wafanya biashara na watendaji wa mamlaka...

MKOMBOZI WA WANAWAKE KUTUMIA HAKI YAO YA DIGITALI.

Image
      NA, AMINA AHMED MOH’D-PEMBA.  ZAITUNI  Abdulkarim Njovu ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Zaina Foundation inayotetea haki  ya kutumia mitandao ya kijamii kwa wanawake Tanzania.   ZAITUNI NJOVU, MKURUGENZI-ZAINA FAUNDATION.  Taasisi hiyo ambayo makao makuu yake makuu ni Dar es Salam  ilianza harakati hizo  mwaka 2017  na kufika Zanzibar  mwaka 2022. Zaituni  alisema walifikia uamzi wa kuwa na hio taasisi baada ya kugundua kuwepo changamoto nyingi, ikiwemo ya ukatili wa kijinsia mtandaoni.   Vile vile zipo changamoto za kiuchumi, kiwango cha chini cha elimu ya matumizi sahihi ya mtandao na wanawake kidogo kutumia haki hiyo ni. Vile vile sheria sio rafiki kwa mwanamke kukingwa anapofanyiwa udhalilishaji mtadaoni. Kwa mujibu wa takwimu  za sensa ya watu na makazi za  mwaka 2022 Tanzania inayo  wanawake   31,68990 ( asilimia 51) na wanaume ni 30,530,130 (asilimia ...

NJIA WANAZOTUMIA VIJANA WA KIKE KUWA VIONGOZI.

Image
THUWAIBA HABIBU  Kasumba ni kilevi kinachompotezea mtu mwendo sahihi wa kufikiri na kufanya maamuzi. Hii ndio iliopelekea jamii kumueleza mtu mwenye mawazo potofu na anayeukataa ukweli kuambiwa ana kasumba, yaani hajielewi na maamuzi yake hayatautiani na aliyetumia kasumba. Katika jamii wapo watu wenye kasumba katika medani ya siasa na kuona na kutaka wengine waamini kuwa mwanamke hawezi kushika nafasi ya uongozi. Watu hawa hujiona waposahihi kuhukumu au kuchukia wenzao kwa sababu zisizo za msingi na zisiokuwa na mantiki. Kwa muda mrefu ipo kasumba katika jamii ya watu wengine kuona viongozi wazuri ni watu wenye umri wa makamo, watu wazima au vikongwe. Hali hii ndio iliopelekea serikali yetu kuweka nafasi maalum za uongozi kwa vijana kwa njia ya kuteuliwa na katika miaka ya karibuni tumeona vijana wanashajiika kuzitafuta nafasi za kuwa wagombea katika chaguzi za ngazi mbali mbali. Katika hili kundi la vijana, wamo wanawake waliogombea uongozi katika vyama vya siasa na m...

MAUMIVU YA MWANAMKE YAKOMBOA ZAIDI YA WATU 2000 KIUCHUMI.

Image
NA THUWAIBA HABIBU, UNGUJA.  HISTORIA inaeleza kuwa kabla ya kuja  kiongozi wa dini ya Kiislamu, Mtume Muhammad (SAW),  wanawake walionekana kama bidhaa isiyo  thamani. Kwa bahati mbaya, licha ya dini ya Kiislamu kukemea mwendo huo, bado wapo watu  wanaokataa kutambua uwezo na mchango wa mwanamke katika kuiletea jamii maendeleo.  Hali hii pia ilikuwepo hadi mwaka 1996 katika Wilaya ya Kati,  Unguja, ambako wanawake walioachika (wajane)walikuwa wakipitia hali ngumu ya maisha. Baadhi yao wakahadaika na kusahau thamani ya utu wao na kutumia miili yao  kujipatia pesa za kujihudumia wao na watoto walioachiwa baada ya waume kutengana nao. Mwenendo huu ulimsononesha binti mmoja ambaye ndoa yake ilikuwa mpya  na kutokea kupendwa na wenzake. Alisema alijiuliza maswali mengi, mojawapo ni kwa nini shida za maisha ziwapelekee akina mama kupoteza utu na heshima yao katika jamii? Baada ya kuitafakari hali hio aliamua kuanzisha upatu, mfumo maarufu wa kusai...

RC KUSINI PEMBA AWATAKA WAJASIRIAMALI NA WAFANYA BIASHARA KUSHIRIKIANA NA MUNIMS INTERNATIONAL TRADING COMPANY LIMITED (MUNIMS CARGO)KUAGIZA BIDHAA KUTOKA NJE.

Image
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.              WAJASIRIMALI na wafanya biashara  kisiwani Pemba wametakiwa  kuitumia fursa ya kuanzisha  huduma  muhimu zinazohitajika katika jamii kwa  kushirikiana na kampuni zinazoaminika na serikali  katika kuagiza bidhaa mbali mbali nje ya nchi ili kujikomboa kiuchumi na kupata maendeleo waliokusudia .  Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud alipokuwa akizungumza na wafanya biashara  na wajasiriamali  kutoka maeneo mbali mbali kisiwani Pemba  katika mkutano maalum  ulionadaliwa na kampuni ya kuagiza na kusafirisha bidhaa mbali mbali kutoka nchini China kuja Tanzania MUNIMS INTERNATIONAL TRADING COMPANY LIMITED. ( MUNIMS CARGO )  International Trading Company Limited   uliofanyika katika ukumbi wa Tibirinzi Chake Chake.  Amesema  wafanya biashara na wajasiriamali wadogo wanazo fursa katika kukuza ...

MATTAR ATOA NENO KWA WAJASIRIAMALI NA WAFANYA BIASHARA PEMBA AWATAKA PIA KUAGIZA BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI KUPITIA KAMPUNI YA MUNIMS CARGO KWA UHAKIKA ZAIDI KUEPUSHA USUMBUFU.

Image
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.              WAJASIRIMALI na wafanya biashara  kisiwani Pemba wametakiwa  kuitumia fursa ya kuanzisha  huduma  muhimu zinazohitajika katika jamii kwa  kushirikiana na kampuni zinazoaminika na serikali  katika kuagiza bidhaa mbali mbali nje ya nchi ili kujikomboa kiuchumi na kupata maendeleo waliokusudia .  Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud alipokuwa akizungumza na wafanya biashara  na wajasiriamali  kutoka maeneo mbali mbali kisiwani Pemba  katika mkutano maalum  ulionadaliwa na kampuni ya kuagiza na kusafirisha bidhaa mbali mbali kutoka nchini China kuja Tanzania MUNIMS  CARGO  International Trading Company Limited   uliofanyika katika ukumbi wa Tibirinzi Chake Chake.  Amesema  wafanya biashara na wajasiriamali wadogo wanazo fursa katika kukuza uchumi wao na taifa kwa kuanzish...