MATTAR ATOA NENO KWA WAJASIRIAMALI NA WAFANYA BIASHARA PEMBA AWATAKA PIA KUAGIZA BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI KUPITIA KAMPUNI YA MUNIMS CARGO KWA UHAKIKA ZAIDI KUEPUSHA USUMBUFU.
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
WAJASIRIMALI na wafanya biashara kisiwani Pemba wametakiwa kuitumia fursa ya kuanzisha huduma muhimu zinazohitajika katika jamii kwa kushirikiana na kampuni zinazoaminika na serikali katika kuagiza bidhaa mbali mbali nje ya nchi ili kujikomboa kiuchumi na kupata maendeleo waliokusudia .
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud alipokuwa akizungumza na wafanya biashara na wajasiriamali kutoka maeneo mbali mbali kisiwani Pemba katika mkutano maalum ulionadaliwa na kampuni ya kuagiza na kusafirisha bidhaa mbali mbali kutoka nchini China kuja Tanzania MUNIMS CARGO International Trading Company Limited uliofanyika katika ukumbi wa Tibirinzi Chake Chake.
Amesema wafanya biashara na wajasiriamali wadogo wanazo fursa katika kukuza uchumi wao na taifa kwa kuanzisha biashara muhimu ambazo zinahitajika na jamii ya kisiwa cha Pemba lakini bado hazijaanzishwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo upatikanaji wa uhakika wa vifaa kutoka nje ya nchi.
"Ni vyema kuzichangamkia Fursa za kuanzisha biashara zenye tija ambazo zinaumuhimu na zinahitajika na jamii kabla ya fursa hizo kuja kuchukuliwa na wageni, mfano kuanzisha vituo vya GYM maenwo mbali mbali ".
Kuagiza vifaa kutoka nje ya nchi kwa kampuni hii yenye vijana wazawa na wazalendo wanapenda maendeleo ya wajasiriamali na wafanya biashara wadogo ambao kutokana na mitaji yao bado uwezo wa kuagiza moja kwa moja kutoka viwandani ni mdogo niwaase muitumie hii fursa adhimu kwenu ya MUNIMS CARGO ".
Tayari vijana wanauzoefu wa muda mrefu kuagiza kusafirisha na kufuatilia bidhaa mbali mbali kutoka viwanda vya china kuja Tanzania" Alisema Mattar.
Aidha mkuu huyo ameipongeza kampuni hiyo ya MUNIMS CARGO kwa kuonesha uzalendo wa kuisadia serikali katika kurahisisha lengo la kuwainua wafanya biashara na wajasiriamali wadogo kiuchumi kwa kushirikiana nao katika kuagiza bidhaa mbali mbali kwa usalama .
Hata hivyo amewataka vijana kujenga imani kampuni mbali mbali za kizalendo ambazo zinalengo la kusaidia serikali na taifa katika kutimiza malengo yaliowekwa na Serikali.
Afya, Viwanda, Uwekezaji, Uchumi wa buluu, Kilimo, Michezo, Ufugaji, na mengi mengineyo ni miongoni mwa vipaumbele vya Dk Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar wa awamu hii ya 8 kwa wananchi wake, tunapowaona vijana wazawa wanakuwa bega kwa bega na serikali yao kwa kuunga mkono na kuonesha njia kwa wengine kufanikisha malengo hayo ni jambo la faraja kwetu, niwatake ndugu wajasiriamali na wafanya biashara kutoiwacha fursa hii badala yake muitumie ipasavyo kuagiza bidhaa mbali mbali .
Nae Mkurugenzi wa kampuni hiyo Munir Said Sleiman amesema lengo la kuwafikia wajasiriamali kuwapa elimu juu ya namna bora ya kuagiza bidhaa zenyw tija na fursa kupitia kampuni hiyo ni kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabali wafanya biashara hao ikiwemo kutapeliwa na kukosa uhakika wa kufika salama biashara zao wanapoagiza kutoka nchini china sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwainua wajasiriamali na wafanya biashara wadogo kwa ushirika na mmoja mmoja .
Aidha mkurugenzi huyo amefafanua fursa hizo za kuagiza bidhaa kwa wajasiriamali wadogo wadogo ni pamoja na vifaa vya kisasa vya ujenzi, vifaa, vya majumbani, vifaa vya michezo, biashara, vifaa vya matibabu, ufugaji, Pembejeo za kilimo, pamoja na uvuvi ambapo amesema kuwa uhakika kuagiza vifaa hivyo kutoka China kuja Tanzania ni wenye kuaminika na kutambuliwa kisheria.
Nao Baadhi ya wajasirimali waliofika katika mkutano huo akiwemo Asha Omar, Pamoja na Omar Hamad Kombo wameishukuru Kampuni hiyo kwa kuwapa uwelewa juu ya kuagiza na kununua bidhaa kutoka china kuja Tanzania ambapo wamesema uwepo wa kampuni hiyo kutasaidia kupunguza changamoto sambamba na kurahisisha uagizaji wa bidhaa mbali mbali na kupatikana kwa urahisi.
Aidha wameiomba Serikali kupunguza baadhi ya gharama wanapiagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ili kuzidisha ufanisi katika biashara zao.
MUNIMS CARGO INTERNATIONAL TRADING COMPANY LIMITED ni Kampuni ya kusafirisha na kuagiza bidhaa kutoka nchini china kuja Tanzania yenye uzoefu na watendaji wazawa wa Zanzibar ambapo miongoni mwa Bidhaa zinazoagizwa kupitia kampuni hiyo ni pamoja na vifaa vya hospitali, vifaa vya kilimo, Uvuvi, vifaa vya majumbani, maofisini, biashara na nyenginezo.
Mwisho
"
Comments
Post a Comment