Mwanamke awapika wenzake kuwa viongozi
Na Thuwaiba Habibu
Elimu ni mchakato wa kupata ujuzi, kukuza uwezo wa kifikiri na uamuzi na kujitayarisha kiakili kwa maisha bora.
Elimu pia hutoa muongozo wa kumuwezesha mtu kufanya jambo kwa vizuri zaidi na humpa mtu uwezo wa kuwaongoza wenzake.
Vile vile humpa mtu uelewa wa kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya biashara au jambo jengine litalomuwezesha kujiongezea kipato na hata kujiepusha na maradhi au hatari inayoweza kuathiri maisha yake.
Nchi nayo hufaidika kwa kujipatia maendeleo pale ambapo watu wake huwa walioelimika
Katika kijiji cha Bumbwini Makoba, wilaya ya Kaskazini B, Unguja, lilikuwepo kundi kubwa la akaina mama waliokuwa hawana elimu hata ya kusoma na kuandika.
Hali hii iliwaweka nyuma na kutoweza kuwa viongozi, lakini pia hata sauti zao kutosikika kwa mambo yanayowahusu katika maisha yao ya kila siku.
Kutokana na hali ya kuelewa kwamba palikuwa panahitajika elimu ili kuibadili taswira hio ndio kilichompelekea Bi Shida Issa Rashid kuona palikuwa panauhitaji wa kutoa elimua ili wanawake hao waondokane na shida walizokuwa nazo na kuweza kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na ufanisi.
Bi shida ambaye ni mmoja wa wanawake aliyeamua kujitolea kuelimisha wanawake wenziwe na ni mratibu wa wanawake na watoto katika kijiji cha Bumbwini Makoba wilaya ya kaskazini "B", Unguja.
Alisema lengo la kuanzisha elimu ya watu wazima katika kijiji chao ni kutaka kila mtu anaweza kujuwa kusoma na kuandika na kuhesabu
Kwa matazamo wake hio ni hatua ya kwanza muhimu ya kumuwezesha mwanamke kuwa kiongozi na ukosefu wake ndio uliopelekea wanawake kuwa nyuma kushiriki kama viongozi katika jamii.
Alisema elimu inamsaidia mwanamke kujiamini na kuwa na uwezo na ujasiri wa kugombea uongozi.
Bibi huyu alieleza kuwa elimu hiyo hutoa kwa wanawake kwa siku tatu kwa kila wiki, kuanzia Jumapili hadi Jumanne.
Mafunzo hayo huanza saa 10 alasiri baada ya watu kumaliza pirika za kazi zao za kawaida za kila siku.
‘’Nimefanya hivyo ili kila mtu aweze kupata fursa ya elimu kwani ni muhimu kwa kila mtu kwa vile pia itawawezesha wanawake kuweza kuchukua nafasi za kuongozi’’, alisema.
Kwa mtazamo wake wanawake wana kila kigezo cha kuwa viongozi wazuri kwa vile siku zote huwa karibu na jamii na kulewa vyema matatizo yaliopo.
Mafunzo aliyoyatoa yamesaidia watu wengi waliokosa bahati ya kupata elimu walipokuwa wadogo kuweza kusoma na kuandika.
Vile vile elimu hio ya kujua kusoma na kuandika imewafanya wajiamini na kuweza kuondokana na khofu waliokuwa nayo kwa vile walikuwa hawajuwi kusoma wala kuandika.
Wengi wao hivi sasa wanao ujasiri wa kujitokeza mbele ya watu na kuzungumza kwa akujiamini
Alianza na wanafunzi watano na sasa wamefikia 20.
Lakini kazi ya kuweza kutimiza lengo lake la kuwakomboa wanawake wenzake kielimu haikuwa rahisi
Mwana mama huyu alikubana na changamoto nyingi, mojawapo ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia
Alianza na wanafunzi watani na sasa wamefikia 20.
Lakini kazi ya kuweza kutimiza lengo lake la kuwakomboa wanawake wenzake kielimu haikuwa rahisi.
Mwana mama huyu alikubana na changamoto nyingi, mojawapo ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia
Hata hivyo alimua kujitolea na kutumia fedha zake mwenyewe ili kupata baadhi ya hivyo vifaa.
Mmoja wa hao wanafunzi wa darasa la watu wazima , Bi. Navuli Ameir, alisema alishindwa kusome alipokuwa mdogo kutokana na hali duni ya kimaisha katika familia yake.
Lakini baada ya kuwepo mpango wa kufunguliwa darasa la elimu ya watu wazima aliamua kujiunga na kisomo cha elimu ya watu wazima.
‘’Niliona wenzangu wakitoka madrasa ya Quran wanaelekea skuli ila kujipatia elimu
Lakini mimi nilipotaka nipelekwe skuli niliambiwa hapakuwepo uwezo’’, alieleza kwa masikitiko hali ilivyokuwa hata akakosa kwenda skuli alipokuwa mdogo.
Alisema aluumia sana, lakini hakuwa na la kufanya ili naye aweze kwenda skuli kama watoto wenzake.
Alisema aliiambia nafsi yake kuwa ikitokea fursa ya kupata elimu hataiachia ipotee na alishukuru kwamba nafasi hio ilikuja kwa kufunguliwa darasa la elimu ya watu wazima.
Alisema sasa akipata barua anaweza kuisoma na anaweza kuelewa ujumbe uliopo kwenye maandishi.
Alisema awali kabla ya kupata elimu hiyo palikuwa na tangazo ambalo limeandikwa watu wasipite, lakini yeye bila ya kujua kwamba lilikuwepo tangazo la aina hio alipita na akasimamishwa na kupewa onyo baada ya kuomba radhi kwamba alikuwa hajuwi kama ilikuwa hairuhusiwi kupita sehemu hio
Sheha wa Bumbwini Makoba, Khamis Subuki Pande, alisema wanajitahidi kushirikiana na wanawake kuleta maendeleo katika kijiji chao na kuanzishwa kwa masomo ya elimu ya watu wazima ni fursa nzuri ya kuwakomboa akina mama.
Alisema siku hizi wanawake wamekuwa na muamko mkubwa wa kushika nafsi za uongozi katika shehiya yao.
Hii ni hatua nzuri ya wanaume na wanawake kwenda sambamba katika kujitafutia maendeleo
Comments
Post a Comment