Posts

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AIPA KONGOLE HOSPITALI YA KINYASINI KWA HILI

NW MWANDISHI WETU ,WIZARA YA AFYA PEMBA WAZIRI wa afya Zanzibar  Nassor Ahmed Mazrui  amefanya ziara  maalum  katika Hospitali ya  Wilaya  Kinyasini   ambayo ilikuwa na lengo la kuangalia hali ya utoaji wa huduma  kwa wananchi  wanaofika hapo kufata huduma mbali mbali. Ambapo  taarifa ya utendaji kutoka kwa daktari hospitalini  hapo   juu ya mama wajawazito   na watoto wanaozaliwa  ni ya kuridhisha ambapo hakujawahi kutokea kifo chochote cha mama mjazito na watoto. Sambamba na hayo Mazrui pia ametoa maelekezo   kuhusu upatikanaji wa majibu ya maabara  kwa wagonjwa yaweze kutolewa kwa haraka .