WAKULIMA KIUYU WALIA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI
Wakulima wa kilimo mseto katika shehiya ya kiunyu Minungwi wamesema baado wamekuwa wakikabiliana na changamoto ya Majichuvi kwenye maeneo mbali mbali katika shehia hio.
Kaulihio imetolewa na Fatma Shabani Mohamed kwaniaba ya wakulima katika shehiya ya kiuyu Minungwini ambaye piya ni Mwalimu wa Wakulima anaejulikana kama TOT wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wahabari juu
ya kutaka kuzifahamu changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabiya ya nchi katika ahehiya hio.
Amesema baado wapo wanajamii hawanauwelewa wakutosha juu ya kuzijuwa athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabiya ya nchi jambo ambalo linapelekeya kurudishanyuma maendeleo ya wakulima na wanaoishi pembezoni mwabahari.
Akizitaja changamoto hizo nipamoja na kupanda kwa Maji chuvi mpaka majumbani ikiwahukoseaha wananchi kwenda kufanya kazi za kujipatia kipato.
Nae sheha wa shehiya ya chwale Mchanga Said Salim amesema lichayakutolewa elimu ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabiya ya nchi lakini baado kuna wananchi wanafanya hujuma ya kukata miti bila ya kuzingatia athari ambazo zinaweza kujitokeza.
Amesema wamekuwa wakichukuwa jitihada ya kuzibiti ukataji wa miti ili kupunguza athari hizo nakuziunga mkono nguvu za Serekali pamoja na Mradi ambao umewafikia wa ZANZADPT ambao unalengo lakutaka kuwakombowa wanawake juu ya athari zitokokanazo na Mabadiliko ya nchi.
Aidha Ali Omar Ali sheha wa shehiya ya kambini amesema kwaupande wake katika kukabiliana na athari hizo wamekuwa wakichukuwa jitihada ya kuwaunga mkono akina mama ili kuwea kukabiliana na changamoto mbali mbali zikiwemo za Mabadiliko ya Tabiya ya nchi.
Comments
Post a Comment