CCM KUSINI PEMBA YATOA TANO KWA SERIKALI NA VIONGOZI WAKE YAAHIDI MAZURI HAYA 2025
Na,Amina Ahmed Moh'd -Pemba.
KAMATI YA Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Pemba imetoa Pongezi kwa Serikali zote Mbili zinavyoendelea kutekeleza kwa zaidi ya asilimia 100 ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 / 2025 sambamba na kutoa Huduma zenye ubora kwa jamii.
Akitoa Pongezi hizo kwa waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Juma Ali Amesema utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi uliofanywa na Dk Samia Suluhu Hassan Pamoja na Dk Hussein Ali Mwinyi umekuwa chachu ya katika kuleta Maendeleo ya wazi katika sekta zote yanayowanufaisha wananchi Unguja ,Pemba na Tanzania .
Kamati hiyo kwa kushirikiana na wananchama wa chama cha Mapinduzi CCM imesema itaendelea kuunga mkono juhudi za viongozi hao kwa kuwalipa ushindi wa vishindo chama na viongozi hao katika uchaguzi wa mwaka 2025.
Kamati hiyo pia imeiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusimamia suala la kupungua kwa bei za vyakula ikiwemo Mchele ili lengo la maboresho ya Bandari ya Mkoani yaliyochukuliwa yaweze kufikiwa na kuweza kuwanufaisha wananchi kwa vile tayari meli za makontena zimeanza kufika moja kwa moja kutoka Mombasa Hadi kisiwani Humo lakini bado hakuna utofauti katika bei za vyakula zilizokuwepo awali na sasa .
Mkutano huo maalum kwa waandishi wa habari uliofanyika leo disemba 24 katika ukumbi wa Baraza la manispaa Chake chake umefuatiwa na mkutano mkuu wa kamati ya halmashauri kuu ya CCM mkoa huo .
Mwisho.
Comments
Post a Comment