ZNCC Yawafikia wafanya biashara Pemba
Jumuiya ya kitaifa ya wafanyabiashara Zanzibar ZNCC imewafikia wafanyabiashara waliopo kisiwani Pemba na kushirikiana nao katika kuwajengea miundombinu imara Ili kufikia maendeleo endelevu.
Akiwa katika ziara ya kutembelea wafanyabiashara mbali mbali huko wilaya ya mkoani mratibu kutoka jumuiya ya wafanyabiashara ya kitaifa Zanzibar ZNCC Khalfan Amour Muhammed amesema wajasiriamali wengi amesema Bado wajasiriamali hawajitangazi na kuonesha uwezo wao wa kazi katika kufikia viwango ubora vinavyohitajika .
Aidha amesema ZNCC imeandaa mradi ulio kwa lengo la kuwasaidia wafanyabiashara katika Kuwapatia fursa mbali mbali Ili waweze kufikia malengo yao sambamba na kuwakuza kiuchumi.
Wakitoa changmoto zao wajasiriamali hao wamesema kuwa ukosefu wa vitendea kazi umekua ukiwapelea kushindwa kufanya kazi zao Kwa ufanisi.
Aidha wamewaomba wafanyabiashara walioko kisiwani Pemba kuwasogezea karibu malighafi Ili Wendell sambamba na wajasiriamali wengine.
Comments
Post a Comment