WADAU WAANZA KUMUITA HAMISA FURSA KATIKA MICHEZO
NISHAITWA katika mafunzo ya michezo mara mbili siku na wadau tofauti wananipigia simu nilisema nikutafute mwandishi lakini namba yako Ilinipotea na huku nina mambo mengine nikahaflika nashukuru leo tumeonana tena.
Waalimu tunapokuwa katika mazoezi ya vitendo wananikubali sana wananiambia kweli niko fiti na ninauwezo wa michezo Alisema .
Ni maneno ya Hamisa Omar Hamad mwanamichezo kutoka Club ya mazoezo ya viungo Gombani fitness kuanza kufikiwa na fursa za kushirikishwa katika michezo alipokutana na mwandishi wa habari hizi katika uwanja wa Gombani akiwa katika harakati za kuoatiwa mafunzo ya vitendo juu ya kutumia mbinu za michezo kupamabana na vitendo vya udhalilishaji yalioandaliwa na Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Zafela.
Hamisa ambae awali alitamani kupata fursa ya kushirikishwa katika michezo mbali mbali ambayo anaamini kwa utayari wake na uthubutu alionao anaweza kushiriki kuicheza na kuifundisha ambapo kupitia makala iliyochapishwa na mwandishi wa habari hizi aliomba wadau kumshirikisha kuweza kuonesha uwezo wake.
Comments
Post a Comment