ANGOZA YATOA MAFUNZO MABADILIKO TABIA YA NCHI.
NA, ARAFA MAKAME,RAIHAT NASSOR -PEMBA.
AFISA mdhamini wizara ya nchi ofisi ya makamu wa kwanza wa rais Pemba Ahmed Abubakar Mohammed amewataka amesema ipo haja ya kulindwa na kuendelezwa misitu na mapori ili kuhakikisha Kisiwa cha Pemba kinaendelea kubaki na haiba yake ya Kijani .
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wawakilishi wa asasi tofauti za kiraia,Wananchi,watoto watu wenye ulemavu,wanawake pamoja na watendaji wa serikali Pemba uliyoaandaliwa na ANGOZA kwa ufadhili wa mfuko wa jumuiya ya madola COMMON WEALTH FOUNDATION katika kuleta mabadiliko ya tabia ya nchi (CLIMATE JUSTICE) yaliyifanyika huko katkka ukumbi wa Madungu sekondari .
Amesema katika kutekeleza suala hilo jamii inalazimika kuacha ukataji wa miti kiholela na kutumia nishati ambayo nisalama jambo ambalo itapelekea kuharibu mazingira na kupelekea kuwa na vihatarishi vitakavyoleta athari ikiwemo kujaa maji ,katika maeneo ya makazi ya wananchi sambamba na kuzidi kwa kina cha maji ya chumvi katika bahari.
Kwa upande wake Mkurugenzi Kutoka taasisi ya ANGOZA Zanzibar Hassan khamis Juma amewataka wawakilishi wa jumuia na makundi hayo kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii katika kulinda mazingira ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwemo wakina mama, vijana na watu wanaoishi pembezoni mwa bahari sambamba na wakulima wa mwani..
Nae kwa Upande wake katibu mkuu wa Angoza Zanzibar khamis Ngwali Makame amesema lengo la kuanzishwa kwa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watu wa makundi mbali mbali juu ya kutambua athari za uchafuzi wa mazingira na haki ya mabadiliko ya tabia ya ncji ambayo yamekuwa yakiwagusa watu waote.
Amesema Pemba ni miongoni mwa nchi ambayo imeathirika zaidi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo jumla ya maeneo 123 yameshathirika kutokana na mabadiliko hayo kutokana na athari za kimazingira.
Ameongeza kuwa mradi huo pia umegusa mazingira kwa wanawake wanaojishughulisha na kilimo wakiwemo wakulima wa mwani ,ambao pia ni waathirika wakubwa
Katika shughuli zao ,ambapo pia hutumia
miti katika maeneo mbali mbali ya bahari na kupelekea kuharibu mazingira .
Akitoa elimu juu ya athari za kimazingira kwa washiriki hao mkufunzi wa mafunzo hayo Afisa kutoka ofisi ya makamu wa pili wa rais Pemba Salum Hamad Bakar amesema taaluma ya mabadiliko ya tabia ya nchi inayoendelea kutolewa kwa washiriki hao imelenga kuwakumbusha wajibu wao kwa jamii katika kupambana na kuweza kutatua changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi yanapoweza kutokea katika jamii .
Mafunzo hayo yalijumuisha watu mbali mbali wakiwemo wanawake, vijana, Watoto, watu wenye mahitaji maalumu pamoja na watu wanaoishi pembezoni mwa bahari,asasi za kiraia,pamoja na asasi za serikali.
Mwisho
Comments
Post a Comment