KUKOSEKANA FURSA HABARI ZA MICHEZO NDANI YA VYOMBO VYA HABARI KIZINGITI KWA WANAWAKE KUSHIRIKI MICHEZO.
NA AMINA MASOUD, PEMBA.
KUWEPO Kwa nafasi ndogo y kuandikia habari za michezo za wanawake ni sababu inayopolekea kundi Hilo kutoshiriki Kwa wingi katika michezo.
Akizungumza katika muendelezo wa mafunzo ya siku Tano mtaalam wa masuala ya JINSIA ambae pia ni mkufunzi katika mafunzo hayo Hawra Shamte amesema vyombo vya vya habari hutoa nafasi ndogo katika kuandika habari za michezo za wanawake hataa pale mafanikio yanapokuwa makubwa kuliko ya wanaume jambo ambalo linawafanya watu wa kundi Hilo kuona hawana nafasi katika michezo.
Amesema imefika wakati sasa Kwa vyombo vya habari kuweka usawa na usawia katika kuandika na kuripoti habari za michezo Kwa wanawake kwani nao wanahaki sawa na wanaume.
Ameeeleza kuwa endapo vyombo vya habari vitatoa fursa sawa kati wanawake na wanaume katika michezo basi kinaweza kuongoza idadi ya wanawake katika michezo.
Katika hatua nyengine amesema licha ya vyombo vya habari kutokuripoti Kwa kina lakini pia kunachangamoto ya uwakilishi mdogo wa wanawake katika uongozi wa michezo jambo ambalo linachangia kukosekana watu wa kuwatetea.
Amefafanua kuwa Zanzibar inajumla ya vyama vya michezo 42 na kamati ya uongozi yenye wajumbe 14 kati Yao wanawake 5 na wanaume wakiwa 9 ambapo Kwa upande wa primear lingi hakuna kiongozi mwanamke.
Kwa upande wake mratib wa program ya michezo Kwa maendeleo Khairat Haji Ali amewataka waandishi hao kutumia bmbinu mbadala michezo kuandika habari chanya dhidi wanawake na michezo Ili kuleta mabadiliko.
Nao washriki wa mafunzo hayo wamesema kupitia Elimu hiyo na kuona mapungufu yaliyopo katika kuripoti habari za michezo za wanawake wameeahid kuyafanyia kazi na kuona faida inapatikana
Habiba Zarali kutoka gazeti la Zanzibar leo amesema mafunzo hayo yamekuja kiwafumbua macho kwani kuandikia habari za michezo itasaidia wanawake kufaidika katika mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha afya.
Program ya michezo Kwa maendeleo inatekelezwa na TAMWA Zanzibar,ZAFELA pamoj na CYD Kwa kushirikiana na na shirika la Deutsche Gesellschaft for International Zusammenarbeit(GIZ) la ujerumani lengo la program hiyo ni kuhamasisha waandishi kuandika habari za michezo na JINSIA Ili kuongeza idadi ya wanawake katika michezo.
Comments
Post a Comment