VIJANA WATEMA CHECHE SERA ZINAZOBADILIKA BADILIKA Habari
Na Amina Ahmed Moh’d Pemba.
ZAIDI ya Vijana 40 Kutoka maeneo na Taasisi mbali mbali Kusini na Kaskazini mwa kisiwa cha Pemba Leo hii Wameshiriki katika Kongamano Maalum la kujadili Masuala ya kidemocrasia na ushirikishwaji wa Vijana katika Siasa, Democrsia, Jamii na Uchumi, Yalioandaliwa na Kijana High Faundation, Taasisi ya Youth Initiative, Pamoja na Taasisi ya One Young Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake.
Akifungua Kongamano hilo Kwa niaba ya Mrajisi wa Asasi za Kiraia Pemba Sada Abuu - Bakar Muhammed Amewataka Vijana kutumia vyema nafasi ya kushiriki kuleta Maendeleo ya nchi.
Amesema endapo Vijana wataweza kushirikiana ina kuzitumia vyema fursa zinazopatikana katika Nyanja Mbali mbal Bila kujali tofauti zao za Dini, Rangi Mahala wanapotoka, imani itikadi, Pamoja na siasa zao kutapelekea kupatikana Maemdeleo yao na Taifa.
Wakizungumza katika kongamano hilo la Majadiliano Baadhi ya vijana Akiwemo Nassir Juma, Pamoja na Zuleikha Maulid Heri wameiomba Serikali Na Taasisi za Vijana Kusimamia Vyema Masuala ya Sera na Mikakati Inayoanzishwa ili iweze kuwa endelevu kwa Maslahi ya Muda mrefu Kwa Vijana na iondokane na kubadilika badilika.
Akizungumzia kongamano hilo Suleiman Muyuni kutoka Kijana High Faundation amesema Lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha vijana wa kada za aina mbali mbali kuzungumza mambo yanayaowahusu vijana ili kusaidia kushiriki na kutoa Mapendekezo ya kisera, mikakati na sheria kwa Serikali zote mbili ambazo zitasaidia kujenga Tanzania .
Kongamano hilo lililokuwa na Lengo la kuhamasisha ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya Maendeleo hayo Jumla ya Mada Tatu zinazohusu fursa, Maendeleo, chamagamoto na Ushiriki wa vijana ziliwasilishwa na kutolewa Mapendekezo na Washiriki wa Mafunzo hayo.
Mwisho.
Comments
Post a Comment