MKURUGENZI PEGAO AELEZA MAFANIKIO YALIOFIKIWA KUTATUA KERO ZINAZOREJESHA NYUMA WANAWAKE KUFIKIA MAENDELEO YA KUWA VIONGOZI, ASISITIZA MASHIRIKIANO VIONGOZI WA SHEHIA KATIKA KUZIPATIA UFUMBUZI KERO HIZO.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA.
WAANDISHI wa Habari Wameaswa Kutoa Taarifa ambazo zitasaidia kujenga uelewa kwa Jamii Juu ya kupatiwa ufumbuzi changamoto zinazopelekea kutofikia Maendeleo yao kwa Wanawake ikiwa ni Pamoja na kupata Haki katika nafasi za Uongozi.
Ametoa Ushauri huyo Mkurugenzi wa Jumuiya ya PEGAO Kisiwani Pemba Hafidh Abdi Said,alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano Maalum wa kutoa Taarifa kwa vyombo vya Habari juu ya kazi zinazofanywa na wahamasishaji jamii (Citizen Brigadi) katika wilaya uliofanyika katika ofisi za Jumuia hiyo Msingini Chake Chake Ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Kuwajegea Uwezo wanawake katika Masuala ya Uongozi.
Amesema Wanawake na wananchi wamekuwa wakikukabiliwa na changamoto mbali mbali, ikiwemo suala la Maji safi na salama, umeme kwa baadhi ya vijiji, Barabara, madaraja, elimu, vituo vya afya kufuata masafa marefu, changamoto ambazo zinaweza kutatua iwapo Waandishi wa Habari watatumia vyema kalamu zao kwa kushirikiana na Wahamasishaji hao , kuzisemea Changamoto hizo, kupatiwa ufumbuzi na kusaidia Kufikiwa Mlengo ya Uongozi kwa Wanawake .
Katika hatua Nyengine Mkurugenzi Hafidhi alisema Mradi huo kupitia Wahamasishaji jamii umefanikiwa kupatiwa ufumbuzi jumla ya kero 17 katika kipindi kifupi cha uhamaishaji jamii, ambazo zilikuwa zitaathiri zaidi wanawake kufikia lengo lao la kushiriki katika nafasi za uongozi ikiwemo kero za ukosefubwa huduma za Maji safi na salama.
Akizungumza katika Mkutano huo Mratibu wa Tamwa Pemba Fat-hiya Mussa Said, alisema jamii imepata uwelewa wakutosha kutoka kwa wahamasishaji jamii, katika kuibua kero na kuweza kuzitatua, ambapo amewaasa Masheha na viongozi wa serikali kisiwani Peba kushirikiana kwa pamoja kupitia kamati za shehia kwa lengo la kuandaa mikutano, ili kujadili changamoto zinazowakabilia wananchi na kuweza kupatiwa ufumbuzi.
Nae Mratibu wa PEGAO Dina Juma, alisema mradi huo utaendelea kufanikiwa na kufikia Malengo endapo waandishi wa habari ni wataendelea kujikita katika kuandika na kuhamaisha jamii, juu ya kushiriki katika nafasi za Uongozi na Demokrasia.
Mradi huo wa Mradi wa kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya uongozi unaendeshwa na TAMWA-Zanzibar, ZAFELA na PEGAO kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway ambapo jumla ya kero 44 zimeubuliwa na wahamasishaji jamii katika Wilaya zote kisiwani Pemba.
MWISHO.
Comments
Post a Comment