MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.
NA ASIA MWALIM MARA nyingi tumeshuhudia uzinduzi wa mipango mikakati kwenye masuala mbali mbali ikizinduliwa, lakini ukifatilia kwa karibu utabaini utekelezaji wake haufikii lengo husika. Kwa kuwa utekelezaji wake hauzingatiwi, huo huwa wakati kwa baadhi ya watu kutokujali kutekeleza yalioelezwa kutokana kutochukuliwa hatua yoyote. “Huwezi kumwambia mgeni apite wakati mlango wa nyumba yako umeufunga” huu ni wakati sasa serikali, wadau mbali mbali wa michezo na jamii kushirikiana katika utekelezaji wa mpango mkatati jumuishi wa michezo ili kufikia dhana ya kuanzishwa kwake na kila mmoja kunufaika na fursa za michezo. Kwa muda mrefu kundi kubwa la wanawake na wasichana walishindwa kushiriki michezo ipasavyo kutokana na changamoto kadhaa ambazo hazina usalama kwao kushiriki michezo. Hali hiyo ni miongoni mwa vikwazo vinavyowakabili baadhi ya wanawake wanaojitokeza kushiriki michezo, hatimae kuvunja ndoto zao ya kuibua vipaji kwa kut...