Posts

Showing posts from November, 2024

MTU MMOJA MIKONONI MWA POLISI AKITUHUMIWA KUBAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO WA MIAKA SITA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia mtu mmoja aitwae Maulid Hassan Maulid  (18) mkaazi wa Mwera Pongwe katika Wilaya ya Kati,  Mkoa wa Kusini Unguja kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mdogo Khadija Dadi Mhoda (06) mwanafunzi wa chekechea mkaazi wa Mwera Vichaka mabundi, shehia ya ubago. Akizungumza na waandishi wa habari huko Tunguu , Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Daniel Shillah amesema tukio hilo la Mauaji lilitokea Novemba 14, 2024 huko Mwera Vichaka Mabundi ambapo Mtuhumiwa huyo alimwingilia kimwili na kumsababishia kifo chake. Kamanda SHILLAH amesema Jeshi la Polisi Katika Mkoa huo linaendelea kufanya upelelezi ili mtuhumiwa huyo afikishwe Mahakamani.

CHADEMA ZANZIBAR YATUMA NENO KWA VIONGOZI

Na,Amina Ahmed Moh'd Pemba. MAKAMU  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Said Issa Moh`d amelitaka Bazara la viongozi wa chama hicho kanda ya Pemba kufanya kazi kubwa wa kukipambania chama hicho ili kiweze kushinda katika nafasi mbali mbali za uongozi kisiwani humo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Amesema chama hicho kwa sasa kimekuwa kikiendelea kuimarika kila kukicha na kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi hasa vijana, hivyo viongozi hao wakiendelea kufanya kazi nzuri nafasi ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwakani ipo wazi. Issa ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Bazara hilo kanda ya Pemba katika mkutano mkuu wa kanda ulioambana na uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa kanda hiyo uliofanyika huko  Hifadhi Hotel Tibirinzi Chake Chake. Amesema baada ya muda mrefu wa kupambana na kukijenga chama hicho hapa visiwani Zanzibar sasa kina fursa ya kusimamia wagombea katika nafasi mbali mbali na kushindwa kwani tayari kimekubalika k...