SMZ KULISAIDIA JESHI LA POLISI KUKABILIANA NA UHALIFU – WAZIRI HAMZA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma amesema, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar italiongezea nguvu Jeshi la Polisi ili liweze kufanya kazi ya kulinda maisha ya watu na mali zao kwa ufanisi. Akizungumza na Maafisa wa Polisi huko Mahonda Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja mara baada ya kufanya ziara ya ukagua wa Vituo vya Polisi vya Mikoa mitatu ya Unguja yenye lengo la kuangalia changamoto ili zifanyiwe kazi ambapo Mhe. Hamza ameliagiza Jeshi la Polisi kukabiliana na changamoto za uhalifu ukiwemo wa ajali zinazosababishwa na waendesha pikipiki maarufu bodaboda, makosa ya udhalilishaji na makosa dhidi ya raia wa kigeni. Aidha, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaunga mkono Jitihada za Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wanaohatarisha Amani ya Nchi kwa kutoa maneno ya uchochezi na kuwahamasisha wananchi kufanya fujo. Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar CP HAMAD KHAMIS HAMAD ameio...