150 KUSHIRIKI RIADHA WAKIWEMO WANAFUNZI KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA TAREHE 29 MWEZI HUU
Siku ya Mtoto wa Afrika Zanzibar CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Idara ya Michezo, Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Taasisi ya Maendeleo ya Mashirikiano ya Ujerumani (GIZ) na Kituo cha Mijadala kwa Vijana (CYD), inatarajia kuadhimisha ya siku ya kimataifa ya Mtoto wa Afrika tarehe 29 Juni 2024 kwa kuandaa mashindano ya riadha kwa wanafunzi wa skuli mbalimbali za Zanzibar. Maadhimisho hayo yatawahusisha jumla ya washiriki 150 ambapo kati ya hao watakaoshiriki mashindano ni wanafunzi 75 kutoka katika skuli za Unguja ambazo zimeshajiandaa kushiriki mashindano hayo. Tukio hili muhimu ambalo linalenga kuhamasisha usawa wa kijinsia katika michezo litawaleta pamoja wadau kutoka taasisi za kierikali na zisizokuwa za kiserikali ikiwemo wanafunzi kutoka skuli mbalimbali za Unguja, wanamichezo, walimu wa michezo, na wadau wote wa masuala ya usawa wa kijinsia. Maadhimisho haya yanatoa fursa kwa wasichana kuone...