MKURUGENZI PEGAO AELEZA MAFANIKIO YALIOFIKIWA KUTATUA KERO ZINAZOREJESHA NYUMA WANAWAKE KUFIKIA MAENDELEO YA KUWA VIONGOZI, ASISITIZA MASHIRIKIANO VIONGOZI WA SHEHIA KATIKA KUZIPATIA UFUMBUZI KERO HIZO.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA. WAANDISHI wa Habari Wameaswa Kutoa Taarifa ambazo zitasaidia kujenga uelewa kwa Jamii Juu ya kupatiwa ufumbuzi changamoto zinazopelekea kutofikia Maendeleo yao kwa Wanawake ikiwa ni Pamoja na kupata Haki katika nafasi za Uongozi. Ametoa Ushauri huyo Mkurugenzi wa Jumuiya ya PEGAO Kisiwani Pemba Hafidh Abdi Said,alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano Maalum wa kutoa Taarifa kwa vyombo vya Habari juu ya kazi zinazofanywa na wahamasishaji jamii (Citizen Brigadi) katika wilaya uliofanyika katika ofisi za Jumuia hiyo Msingini Chake Chake Ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Kuwajegea Uwezo wanawake katika Masuala ya Uongozi. Amesema Wanawake na wananchi wamekuwa wakikukabiliwa na changamoto mbali mbali, ikiwemo suala la Maji safi na salama, umeme kwa baadhi ya vijiji, Barabara, madaraja, elimu, vituo vya afya kufuata masafa maref...