Posts

Showing posts from July, 2024

KAZI 162 ZINAZOHUSU SHERIA YA HABARI NA UHURU WA KUJIELEZA ZIMECHAPISHWA.

NA ASIA MWALIM  JUMLA ya kazi 161 zinazohusu sheria ya habari na uhuru wa kujieleza zimechapishwa na waandishi wa habari 25 wa Unguja na Pemba waliopatiwa mafunzo kupitia mradi wa miaka 2 wa majaribio wa mapitio ya sheria za habari Zanzibar. Afisa Programu wa mradi wa majaribio wa mapitio ya sheria za habari Zanzibar kutoka TAMWA Zaina Abdalla Mzee, aliyasema hayo wakati akiwasilisha ripoti ya tathmini ya utekelezaji wa mradi kwa kipindi cha mwaka mmoja 2023/2024 kwa waandishi wa habari, wadau wa serikali na binafsi wakiwemo ZAMECO na tume ya Utangazaji Zanzibar.  Alisema kazi zilizowasilishwa zilionyesha mapungufu yaliyojitokeza katika sheria mbali mbali za habari ikiwemo sheria namba 5 ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magaazeti na Vitabu ya mwaka 1988 na marekebisho yake namba 8 ya mwaka 1997 ambayo ni ya muda mrefu. Na sheria namba 7 ya mwaka 1997 ya Tume ya Utangazaji Zanzibar, na marekebisho yake namba moja ya mwaka 2010 ambazo bado zina wakwaza waandishi wa habari katika ...