KUKOSEKANA FURSA HABARI ZA MICHEZO NDANI YA VYOMBO VYA HABARI KIZINGITI KWA WANAWAKE KUSHIRIKI MICHEZO.
NA AMINA MASOUD, PEMBA. KUWEPO Kwa nafasi ndogo y kuandikia habari za michezo za wanawake ni sababu inayopolekea kundi Hilo kutoshiriki Kwa wingi katika michezo. Akizungumza katika muendelezo wa mafunzo ya siku Tano mtaalam wa masuala ya JINSIA ambae pia ni mkufunzi katika mafunzo hayo Hawra Shamte amesema vyombo vya vya habari hutoa nafasi ndogo katika kuandika habari za michezo za wanawake hataa pale mafanikio yanapokuwa makubwa kuliko ya wanaume jambo ambalo linawafanya watu wa kundi Hilo kuona hawana nafasi katika michezo. Amesema imefika wakati sasa Kwa vyombo vya habari kuweka usawa na usawia katika kuandika na kuripoti habari za michezo Kwa wanawake kwani nao wanahaki sawa na wanaume. Ameeeleza kuwa endapo vyombo vya habari vitatoa fursa sawa kati wanawake na wanaume katika michezo basi kinaweza kuongoza idadi ya wanawake katika michezo. Katika hatua nyengine amesema licha ya vyombo vya habari kutokuripoti Kwa kina lakini pia kunachangamoto ya uwakilishi mdogo wa wana...