MAHAFALI YA PILI WAANDISHI CHIPUKIZI (YMF) YAMEFANYIKA LEO WAASWA KUENDELEZA HAYA
AMINA AHMED MOH'D. SHEREHE ya mahafali ya pili kwa waandishi wa habari chipukizi Young media fellowship (YMF) imefanyika leo katika ukumbi wa Bima Kisiwani Unguja ambapo jumla ya wahitimu 24 waliopatiwa mafunzo kwa muda wa mwaka mmoja kupitia mradi wa kuandika habari zenye kuimarisha uongozi kwa wanawake kupitia vyombo vya habari wamepatiwa vyeti maalum . Akizungumza na wahitimu hao kupitia Sherehe hiyo iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar kwa ufadhili wa shirika la National endowment for democracy ( NED) mkurugenzi wa chama hicho Dk Mzuri Issa Ali amewataka waandishi hao kuendelea kushirikiana na chama hicho katika kutetea haki za wanawake ili kuweza kupata haki wanazostahiki ikiwemo masuala ya uongozi Awali akizungumza Mjumbe wa bodi kutoka Tamw...