Posts

Showing posts from January, 2024

BIDII YAMUWEZESHA KUONGOZA HOTELI KUBWA

Image
NA, THUWAIBA HABIBU, UNGUJA TUNAAMBIWA  mwenye kujitahidi hufaulu na hili limeonekana kwa mwnamke, Sylvia Godleven Moshi ambaye sasa anaongoza hoteli ya Golden Tulip Stone Town Boutique iliyopo Malindi, Unguja. Hoteli hii iliopo karibu na bandari mbali ya kupokea watalii kutoka nchi mbali mbali ni kituo maarufu cha mikutano. Mwanamke huyu ana miaka 25, lakini bidii zake za kujifunza ,kujiamini na ujasiri zimepelekea licha ya kuwa na umri mdogo kuaminiwa na kupewa dhamana hii kubwa ya kuwangoza wanaume na wanawake zaidi ya 80. Kumbuka kuwa hawa wafanyakazi ni watu wa rika, tabia na mtazamo wa maisha tafauti. Kama utafanya upelelezi wa kupitia hoteli  nyengine za aina hii utaona uongozi wa hoteli wa nafasi hii amepewa mtu mwenye umri mkubwa kidogo, uzoefu wa muda mrefu wa kazi ya hoteli na wengi wao ni mwanamume. Lakini mwana dada huyu  amefanikiwa kuwa kiongozi wa hii hoteli kutokana na bidii ya kujituma na kujenga maelewano mazuri na wafanyakazi na wateja wana...