SEA CLIF YAFANYA HAYA KWA WATOT O YATIMA MAZIZINI
NA ASIA MWALIM VIONGOZI wa Sea Clif Resort Zanzibar, wameishauri jamii kujenga utamaduni wa kuwapenda na kuwatunza watoto yatima ili wajisikie faraja kama watoto wengine. Meneja Hifadhi kutoka hoteli ya Sea Clif Resort, Zainab Othman, aliyasema hayo wakati wakikabidhi vyakula na vifaa mbali mbali kwa watoto yatima huko, Mazizini Unguja. Alisema, kufanya hivyo ni moja ya kuwaonesha upendo ili kusahau upweke wa kupoteza wazazi wao na watu wa karibu. Aidha alisema wameamua kutembelea watoto yatima kutokana na upendo walionao kwa watoto hao, sambamba na kuunga mkono Serikali katika kuhakikisha watoto hao wanaishi mazingira mazuri. Miraji Ismail, mfanyanyakazi wa hoteli ya Sea Clif, alishauri wazazi kuacha tabia ya kutelekeza watoto baada ya kuwazaa badala yake kuwalea watoto na kuwapa mahitaji muhimu. Afisa Hifadhi ya mtoto Idara ya Usatawi Jamii na Wazee, Ramadhan Mohammed Ramadhan alisema wamefarijika kutembelewa na viongozi wa hoteli hiyo jambo ambalo limeas...