Posts

Showing posts from February, 2024

TAMWA YATOA WITO KWA WADAUWA HABARI KUZIIANGALIA UOYA SHERIA

na Asya mwalim MKURUGENZI wa Chacha cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzanian, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Dkt. Mzuri Issa, amehimiza vyombo vya habari kuripoti kwa kina mapungufu ya sheria za habari Zanzibar ili zifanyiwe marekebisho na kutoa fursa kwa wananchi kupata habari bila vikwazo. Akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha uzinduzi wa ripoti ya mapitio ya sheria za habari zenye vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari Zanzibar , alisema iwapo vyombo vya habari vitapaza sauti kwa pamoja kushawishi mabadiliko itachochea kasi ya marekebisho ya sheria hizo. "Waandishi wa habari tutumie nafasi kupaza sauti zetu juu ya mapungufu ya kisheria yaliyopo ili zifanyiwe marekebisho, hii itawapa watu furaha na kujisikia kuwa ni sehemu ya nchi kwa kutoa maoni yao bila hofu,"  alieleza Dkt. Mzuri Issa, Mkurugenzi TAMWA ZNZ. Alibainisha waandishi wa habari wakiwa na uwezo wa kutoa maoni yao bila hofu itarahisisha upatikanaji wa taarifa na kuongeza uwajibikaji katika nyanja mbalimbal....